• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Tanzania: Wakulima wapewa msaada

    (GMT+08:00) 2019-08-27 19:19:48
    Kampuni inayojihusisha na ununuzi wa mpunga wilayani Kyela mkoani Mbeya, Kyela Rice Company Ltd, imetoa msaada wa pawatila tisa zenye thamani ya shilingi milioni 134, lengo likiwa ni kuwasaidia wakulima kutumia teknolojia za kisasa kwenye kilimo chao. Msaada huo umetolewa kwa vikundi tisa vyenye wakulima 120, na kampuni hizo zimekuwa zikiwajengea uwezo wakulima namna bora ya kuandaa mashamba. Akitoa msaada huo mwishoni mwa wiki, Mkurugenzi wa kampuni hiyo Moses Mwaipopo,alisema waliamua kutoa msaada huo kwa vikundi hivyo baada ya wakulima hao kuonyesha nia ya kutaka kulima kilimo cha kisasa na chenye tija. Wakulima walishauriwa kuwatumia maofisa ugani waliopo kwenye maeneo yao ili kupata ushauri wa kitaalamu na kuongeza uzalishaji wa mpunga.
    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako