• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Tanzania: Wafanyibiashara watatkiwa kuhama

    (GMT+08:00) 2019-08-27 19:20:13
    Wafanyibiashara zaidi ya 780 wa soko kuu jijini Mwanza nchini Tz, wamepewa makataa ya siku 10 kuanzia hiyo jana hadi Septemba tano mwka huu, wawe wamehamia soko la muda la Mbugani kupisha ujenzi wa soko jipya la kisasa. Amri hiyo imetolewa na Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana, Dk Philis Nyimbi alipotembelea soko hilo ambapo amesema mpango huo unalenga siyo tu kuipa soko hilo hadhi ya kimataifa kulingana na hadhi ya jiji, bali pia itatoa fursa kwa wafanyibiashara wengi zaidi kulinganisha na waliopo sasa.

    Soko hilo jipya litakuwa na jengo la ghorofa mbili lenye vyumba 500 vya biashara, na vizimba 1,500 pamoja na eneo la kuegesha magari zaidi ya 500 kwa wakati mmoja. Soko kuu la sasa lina vizimba 520, maduka 178,bucha 14, migahawa 21,sehemu za kupanga biashara ya ndani ya soko 47, na maeneo kadhaa ya kupanga biashara nje linalotumiwa na wafanyibiashara wadogo wadogo almaarufu wamachinga.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako