• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Uganda: Ugomvi wadunisha biashara kwenye mipaka wa Rwanda

    (GMT+08:00) 2019-08-27 19:21:58
    Ugomvi kati ya Rwanda na nchi jirani wake umesababisha kudorora kwa biashara ambayo sio rasmi mpakani, almaarufu informal cross-border trade. Kulingana na ripoti ya benki kuu nchini humo, mapato ya kuuza bidhaa nje yamepungua kwa asilimia 8.1 huku mapato ya kuagiza bidhaa kuto nje yakipungua kwa asilimia 40 kufikia nusu ya mwaka wa 2019, ikilinganishwa na kipindi kama hicho mwaka uliopita.

    Kwa jumla biashara amabzo si rasmi au hazifuati taratibu zilizopo, huchangia asilimia 10 ya bidhaa ambazo huuzwa nje ya taifa la Rwanda. Uagizaji wa bidhaa kutoka nje ya taifa la Rwanda kwa njia isiyo rasmi huchangia asilimia 0.5 kwa bidhaa zote ambazo huagizwa kutoka nje. Kwa miaka mingi biashara hii imekuwa nguzo muhimu kwa jamii zinazoishi kwenye maeneo ya mipaka ya Rwanda na mataifa jirani.

    Hata hivyo, hali ya ugomvi wa utata uliopo kati ya Kigali na Kampala, iliwaathiri wafanyibiashara hawa kwa sababu ya Rwanda kuamua kufunga mpaka wake na Uganda. Hatua hii iliwazuia wafanyibiashara wa Rwanda kuchuuza bidhaa zao nchini Uganda na Rwanda mtawalia. Hali kama hii pia ilishuhudiwa kwenye ugomvi kati ya Rwanda na Burundi na kuwaathiri wafanyibiashara wanaoishi kwenye mpaka kati ya mataifa haya mawili.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako