• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Rwanda: Marufuku kwa vyakula kutoka nje bado yangalipo

  (GMT+08:00) 2019-08-27 19:39:40

  Serikali ya taifa la Rwanda imesisitiza kwamba bado marufuku ya kupinga kuagiza vyakula kama vile nyama, bidhaa za maziwa na mboga kutoka Afrika Kusini bado yangalipo. Rwanda ilipiga marufuku uagizaji wa bidhaa hizi miaka miwili iliyopita kutokana na mkurupuko wa ugonjwa wa sumu ya chakula unaosababishwa na bakteria.

  Rwanda inasema kwamba inasubiri mwelekeo wa taasisi inayojulikana vyema duniani kutangaza kwamba vyakula kutoka Afrika Kusini ni salama kwa matumizi ya binadamu. Hii ndio njia ya pekee Rwanda itaanza kuagiza vyakula kutoka Afrika Kusini.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako