• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Shirikisho la IFRC latoa mwito wa uaminifu na uelewa zaidi kwenye jamii zinazokumbwa na Ebola, DRC

  (GMT+08:00) 2019-08-28 08:34:40

  Shirikisho la Kimataifa la Mashirika ya Msalaba Mwekundu na Hilali Nyekundu (IFRC) jana lilionya kuwa, licha ya chanjo na matibabu ya ufanisi, kujenga uaminifu na uelewa kwenye jamii zinazokumbwa na ugonjwa wa Ebola nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo ni muhimu sana.

  Onyo hilo limekuja wakati idadi ya vifo vinavyotokana na mlipuko wa Ebola nchini DRC vinakaribia 2,000 huku idadi ya jumla ya wagonjwa ikifikia 3,000.

  Mkurugenzi wa afya na huduma za matibabu wa IFRC Emanuele Capobianco amewataka wagonjwa wa Ebola waziamini dawa pamoja na wafanyakazi wa matibabu wanaotoa dawa hizo.

  Shirikisho hilo limesema, kutoamini huko kumewafanya wagonjwa wengi wa Ebola wachelewe au kuepuka kwenda vituo vya afya, hali ambayo itapunguza fursa yao ya kuishi, hata kama watapata matibabu mapya.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako