• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • SOKA: Rais wa Barca, wajumbe wa bodi wamfuata Neymar Jr na mkwanja mrefu

    (GMT+08:00) 2019-08-28 08:39:17
    Wajumbe wa bodi ya klabu ya Barcelona ya Uhispania kwa mara nyingine tena wamesafiri kwenda jiji la Paris Ufaransa kujaribu kukamilisha dili ama mpango wa kumrudisha Neymar Jr huko Nou Camp.

    Rais wa klabu ya Barcelona, Josep Maria Bartomeu pamoja na mkurugenzi wake, Eric Abidal wamesafiri kueleke makao makuu ya klabu ya Paris Saint-Germain jana Jumanne kuangalia uwezekano huo endapo kama watafikia makubaliano.

    Miamba hiyo miwili ya La Liga wanapambana kufa na kupona kuhakikisha wanamrejesha Mbrazil huyo ndani ya klabu ya Barcelona na sasa wamemuandalia dau la mwisho la dola za Marekani milioni 155 kwa msimu ujao wa usajili huku mipango iliyopo kwa sasa ni kumng'oa kwa mkopo ili kuepuka rungu la FIFA kuhusu matumizi makubwa ya fedha za usajili baada ya kumvuta Griezmann.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako