• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kiongozi wa Zimbabwe asema utawala wa sheria ni kwa ajili ya wote

    (GMT+08:00) 2019-08-28 20:15:24

    Rais Emmerson Mnangagwa wa Zimbabwe amesema utawala wa sheria nchini Zimbabwe unatumika sawa kwa wananchi wote, ikiwa ni pamoja na mashirika yanayopatiwa fedha na nchi za nje.

    Akijibu swali kuhusu hatua zinazochukuliwa na serikali dhidi ya wapinzani, Rais Mnangagwa ambaye yuko ziarani nchini Japan kuhudhuria mkutano wa kimataifa wa Tokyo kuhusu maendeleo ya Afrika (Ticad 7), Rais Mnangagwa amesema hakuna "vigezo viwili" linapokuja suala la utekelezaji wa utawala wa sheria nchini Zimbabwe.

    Kumekuwa na malalamiko kutoka kwenye chama kikuu cha upinzani MDC na baadhi ya mashirika yasiyo ya kiserikali, kuhusu maandamano yaliyopangwa kufanyika kuanzia katikati ya mwezi huu, lakini yalipigwa marufuku na polisi kutokana na sababu za kiusalama.

    Rais Mnangagwa amesema hakuna tukio hata moja la ukiukaji wa haki za binadamu, na kusema kufuata utawala wa sheria hakuna maana ya kuwafurahisha watu wa nje, bali ni jambo zuri kwa Zimbabwe.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako