• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Uganda: Biashara nyingi uganda hazitumii Kiwango cha Kimataifa cha Kuripoti Fedha

    (GMT+08:00) 2019-08-28 20:21:11
    Nchini Uganda Utafiti umeonyesha kuwa ni asilimia 35 tu wafanyabiashara wadogo na wale wa wastani wanaofuata Kiwango cha Kimataifa cha Kuripoti Fedha.

    Mfumo huo ulitolewa na Taasisi ya Wahasibu wa Umma wa miaka tisa iliopita.

    Hayo yamebainika kufuatia kufanyika kwa utafiti uliopewa jina: 'viwezeshaji na Vizuizi vya Ukuaji wa biashara nchini Uganda.

    Utafiti huo ulifanywa na Dr Mary Maurice Nalwoga Mukokoma, mkuu wa idara, Fedha na Uhasibu katika Chuo Kikuu cha Kyambogo na Profesa Charles Tushabomwe wa Chuo Kikuu cha Sayansi na Teknolojia cha Mbarara.

    Kulingana na matokeo, ni asilimia 35 tu ya biashara SME nchini Uganda ambazo hutumia kikamilifu na kufuata mahitaji yote katika kiwango.

    Asilimia 54 wamechukua sehemu tu ya viwango hivyo lakini asilimia 11 ya biashara ndogo nchini nchini Uganda hazijapitisha kiwango hicho .

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako