• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rwanda: Serikali na Afrika 50 kushirikiana ujenzi wa Jiji la uvumbuzi la Kigali

    (GMT+08:00) 2019-08-28 20:21:29
    Serikali ya Rwanda na kampuni ya uwekezaji ya miundombinu Afrika50 zitaunda kampuni ya ubia ambayo itahusika katika kuendeleza, kufadhili, kujenga na kuendesha vyombo vya kibiashara vya Jiji la uvumbuzi la Kigali.

    Africa50 ni kampuni ya kufadhili miradi ya miundombinu barani Afrika iliyoanzishwa na Benki ya Maendeleo ya Afrika, na serikali tofauti za Afrika.

    Makubaliano yaliyosainiwa Jumanne na Bodi ya Maendeleo ya Rwanda yanayowakilisha serikali yanahusisha serikali kugharamia ardhi na na miundo mbinu kama barabara, taa, usambazaji wa umeme.

    Kulingana na makubaliano, halmashauri ya maendeleo ya Rwanda RDB pia itahakikisha uwezeshaji wa jumla ambao unasaidia ushiriki i wa sekta binafsi.

    Tayari Afrika 50 imetangaza kuwekeza katika eneo la kisasa la ujenzi wa jiji la Kigali lenye vipengele 11 na fursa za uwekezaji zenye thamani ya karibu dola milioni 420.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako