• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Tanzania: Wakulima Kilimanjaro kupata mbolea tani 1,200

    (GMT+08:00) 2019-08-28 20:22:26
    Naibu Waziri wa Kilimo, Omari Mgumba, amesema serikali inakusudia kuupatia mkoa wa Kilimanjaro tani 1,200 za mbolea ya kupandia na kukuza mazao mbalimbali ya chakula na biashara.

    Amesema hadi kufikia sasa zaidi ya tani 400 zimeshawasili mkoani humo kwa kutumia treni ya mizigo iliyozinduliwa Julai, mwaka huu, na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa.

    Mgumba aliyasema hayo wakati wa kongamano la Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) Mkoa wa Kilimanjaro.

    Naibu Waziri huyo alisema mkoa wa Kilimanjaro pia umepatiwa zaidi ya lita 2,000 za dawa mbalimbali za viuatilifu kwa ajili ya kupambana na wadudu waharibifu wa mazao mashambani.

    Udhibiti wa wadudu waharibifu wa mazao kwa kutumia viuatilifu, hugharimu fedha nyingi kwa mkulima na hivyo kumlazimu kupambana nao ili kupata mavuno.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako