• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • SOKA: Wadau waipongeza Gor Mahia kusonga mbele CAF

    (GMT+08:00) 2019-08-29 08:47:16
    Wadau mbalimbali wa soka nchini Kenya akiwemo kocha mpya wa Gor Mahia Muingereza Steven Pollack wameipogeza timu ya Gor Mahia nchini humo kwa ushindi wake wa goli 5-1 dhidi ya Aigle Noir ya Burundi, mchezo wa marudiano kuwania kufuzu hatua ya makundi ya michuano ya kombe la shirikisho barani Afrika.

    Wakicheza nyumbani baada ya kutoka sare tasa ugenini jijini Bujumbura, Gor Mahia walicheza mchezo wa kuelewana na hatimaye kupata ushindi huo mnono kupitia kwa mshambuliaji wao Nicholas Kipkurui aliyekuwa mwiba kwa kupiga hat trick.

    Akifunguka baada ya mchezo huo, Pollack amesema kilichosaidia ushindi ni mazoezi mazuri ambayo wamekuwa wakiyafanya kwa wiki nzima. Gor Mahia sasa itakutana na USM Algeirs ya Algeria kati ya Septemba 13 hadi 15 kwenye raundi ya pili ya mchujo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako