• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rais wa Zanzibar Dk Shein asema wajasiriamali wanafaa kusaidiwa kufikia malengo yao

    (GMT+08:00) 2019-08-29 19:50:46

    Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein ameeleza kuwa nia ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar ni kuhakikisha sauti za Wajasiriamali zinasikika na zinafanyiwa kazi ili kufikia malengo waliyoyakusudia.

    Rais Dk. Shein aliyasema, Ikulu mjini Zanzibar alipokutana na uongozi wa Wizara ya Biashara na Viwanda wakati ilipowasilisha Mpango Kazi wa Julai 2018 hadi Juni 2019 sambamba na Mpango Kazi wa Utekelezaji kwa mwaka 2019/2020.

    Alieleza kuwa matajiri walio wengi duniani walianza na ujasiriamali hivyo ni vyema wajasiriamali wakapewa kipaumbele katika shughuli zao wanazozifanya ili waweze kupata mafanikio na kufikia malengo yao waliyoyakusudia ikiwa ni pamoja na kuwashirikisha kikamilifu katika maonesho ya kibiashara ya ndani na nje ya nchi.

    Aidha, Rais Dk. Shein alisisitiza haja ya kuwasaidia wajasiriamali ili na wao waweze kuwa wafanyabiashara wakubwa na kufikia malengo waliojiwekea jambo ambalo limeiibua Serikali katika kuhakikisha inawatekelezea matakwa yao na kuwashirikisha kikamilifu

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako