• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kamishna Mkuu wa KRA,James Mburu, awaonya wanaokwepa kulipa ushuru

    (GMT+08:00) 2019-08-29 19:51:05
    Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya ukusanyaji Mapato nchini Kenya (KRA) James Gathii Mburu amewaonya wanaokwepa kulipa ushuru.

    Mburu amaeyasema hayo wakati ambapo wasiwasi umetanda katika ofisi za KRA ,kwani baadhi ya maafisa wa Shirika hilo wanachunguzwa kwa tuhuma za kuhusika na uhalifu wa kuwasaidia wafanyabishara kukwepa kulipa ushuru.

    Onyo lake pia linajiri siku kadhaa baada ya mkurugenzi mkuu wa kiwanda cha kutengenezea vileo cha Keroche mjini Naivasha, Tabitha Karanja na mumewe John Karanja, kukamatwa na kufikishwa mahakamani kwa madai ya kukwepa kulipa kodi.

    Mnamo Jumanne, Kamishna Mburu alisema takribani kiasi cha Sh250 bilioni, ushuru, ndicho kinakisiwa kukwepwa kulipwa.

    Alisema baadhi ya kampuni na mashirika yamekuwa yakitoza wafanyakazi ushuru, pamoja na kutoa huduma kwa gharama ya mlipa ushuru, bila kulipa kodi yoyote kwa serikali.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako