• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Kenya yapata kifaa kipya cha uchambuzi wa vinasaba DNA cha kupambana na uhalifu

  (GMT+08:00) 2019-08-30 08:43:13

  Kenya imepata kifaa kipya cha kuangalia vinasaba DNA kitakachosaidia nchi kupambana na uhalifu.

  Akiongea na wanahabari mjini Nairobi, waziri wa usalama wa ndani dokta Fred Matiang'i amesema kifaa hicho cha uchambuzi wa jeni aina ya 3500xL ni cha hali ya juu kwa ajili ya uchambuzi wa vinasaba katika kutambua uhalifu na kupima uzazi. Amebainisha kuwa Kenya hivi sasa imejiunga na nchi za dunia ya kwanza kwa kutoa huduma za hali ya juu za uchunguzi na teknolojia ya vinasaba kwa ajili kuwatambua wahanga wa majanga na kukusanya ushahidi kwa ajili ya kuhukumu kesi za uhalifu na usuluhishi wa mizozo ya kumtambua baba wa mtoto.

  Dokta Matiang'i amesema Kenya imekuwa ikisumbuka sana na mlundikano wa data za uchambuzi wa vinasaba, jambo lililopelekea kuchelewa kufikia ufumbuzi kwa kesi nyingi za uhalifu na za mahakama ya kiraia.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako