• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rais wa Uturuki asema hatairuhusu Marekani kuahirisha mpango wa Eneo Salama nchini Syria

    (GMT+08:00) 2019-08-30 08:59:44

    Vyombo vya habari vya Uturuki jana viliripoti kuwa, rais Recep Tayyip Erdogan amesema, hatairuhusu Marekani kuahirisha mpango wa kuanzisha Eneo Salama kaskazini mwa Syria.

    Rais Erdogan amesema, makubaliano yaliyofikiwa na Uturuki na Marekani kuhusu kuanzisha Eneo Salama nchini Syria ni hatua sahihi, mpango huo utasaidia kuondoa vikosi vya kikurdi vya YPG vilivyoko kwenye mipaka kati ya Uturuki na Syria, na kulinda usalama wa mipaka kusini mashariki mwa Uturuki.

    Pia amesisitiza kuwa Marekani ilichelewa mara nyingi kutekeleza mpango wa kuondoa vikosi vya YPG huko Minbic nchini Syria, na mara hii hatairuhusu Marekani kuahirisha mpango wa kuanzisha Eneo Salama kaskzini mwa Syria.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako