• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Shirika la ndege la Ethiopia lapongeza kuanzishwa kwa huduma za kutoa viza kwenye mtandao

  (GMT+08:00) 2019-08-30 09:00:12

  Shirika la ndege la Ethiopia jana limepongeza kuanzishwa kwa jukwaa la kutoa viza kupitia mtandao wa Internet, kwa ajili ya kujenga mustakbali wa nchi hiyo kuwa kituo cha mikutano ya kimataifa.

  Taarifa iliyotolewa jana na shirika hilo limesema, katika miaka kadhaa iliyopita, Ethiopia imechukua hatua nyingi ili kuufanya usafiri uwe rahisi na mwepesi, na uzinduzi wa huduma za kutoa viza kwenye mtandao kwa wasafiri wote wa kimataifa ni hatua kuu.

  Taarifa hiyo pia imesema, huduma za kutoa viza kwenye mtandao ni sehemu ya mpango wa Ethiopia wa kuboresha sekta ya utalii nchini humo. Kutokana na huduma hizo, watalii wa kimataifa watafurahia utaratibu wa viza ambao utaokoa muda wao, nguvu na gharama zao.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako