• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • SOKA: Michuano ya kufuzu kombe la Dunia 2022: Burundi waipania Tanzania, waendelea kujifua nguvu

    (GMT+08:00) 2019-08-30 09:22:18
    Timu ya taifa ya Burundi inaendelea na mazoezi ya kujiandaa kuikabili timu ya taifa ya Tanzania (Taifa Stars) katika mchezo wa kufuzu kombe la dunia mwaka 2022 nchini Qatar utakaopigwa Septemba 4 jijini Bujumbura Burundi.

    Nao Taifa Stars wameanza mazoezi katika uwanja wa Boko Veterani jijini Dar es Salaam.

    Kocha mkuu wa Burundi, Alain Oliever Niyungeko ametangaza kikosi cha wachezaji 29 ambacho kitaikabili Taifa Stars. Burundi watakuwa wenyeji wa Tanzania mchezo huo utapigwa kwenye uwanja wa Intwari, kabla ya kukutana tena katika mchezo wa marudiano utakaopigwa jijini Dar es Salaam Septemba 7.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako