• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Putin na Merkel wapenda kusukuma mbele mkutano wa Normandy Four

    (GMT+08:00) 2019-08-30 09:31:49

    Rais Vladimir Putin wa Russia amezungumza na chansela wa Ujerumani Bibi Angela Merkel kwa njia ya simu na kusema, anapenda kufanya maandalizi kwa ajili ya mkutano ujao wa nchi za Normandy Four kuhusu utatuzi wa suala la Ukraine.

    Tovuti ya Ikulu ya Russia Kremlin imetoa taarifa kuwa viongozi hao wamejadiliana kuhusu mustakabali wa utatuzi wa mgogoro wa Ukraine na kusisitiza kuwa makubaliano ya Minsk ni msingi katika kutatua suala hilo. Pia pande hizo mbili zimekubaliana kusukuma mbele kazi za baadaye chini ya mfumo wa Normandy Four.

    Aidha, msemaji wa serikali ya Ujerumani Steffen Seibert amesema, bibi Merkel anatarajia kuendelea kusukuma mbele utekelezaji wa makubaliano ya Minsk kwa kupitia mkutano huo ujao.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako