• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Iran yaihimiza Marekani kurudi kwenye makubaliano kuhusu suala la nyukilia

    (GMT+08:00) 2019-08-30 09:50:57

    Waziri wa mambo ya nje wa Iran Javad Zarif amesema kama Marekani ikitaka kufanya mazungumzo na Iran, ni lazima irudi kwenye makubaliano yaliyofikiwa mwaka 2015 kuhusu suala la nyukilia, na kuondoa vikwazo dhidi ya ya nchi hiyo. Zarif amesema Marekani inafanya vita vya kiuchumi dhidi ya watu wa Iran, na haiwezekani kwa Iran kuzungumza na Marekani hadi itakapomaliza vita hivyo na ugaidi wa kiuchumi dhidi ya wairan. Mwaka jana rais Donald Trump wa Marekani alitangaza kujitoa kwa nchi hiyo kwenye makubaliano ya nyuklia ya Iran, na kuweka vikwazo dhidi ya Iran. Hivi karibuni Marekani inataka kufanya mazungumzo na Iran, lakini imekataliwa.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako