• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Marekani yatangaza rasmi kuzindua makao makuu ya anga ya juu

    (GMT+08:00) 2019-08-30 18:49:55

    Rais Donald Trump wa Marekani ametangaza kuzindua rasmi makao makuu ya anga ya juu, na nchi hiyo imepiga hatua ya kukaribia kuunda jeshi la anga ya juu.

    Rais Trump amesema, uzinduzi huo umeonesha hadhi muhimu ya anga juu katika usalama wa taifa na ulinzi wa taifa wa Marekani, ambao utahakikisha hadhi ya kutawala anga ya juu ya Marekani kutoshukiwa na kutotishiwa. Kamanda wa makao makuu ya anga ya juu ya jeshi la anga la Marekani John Raymond atakuwa kamanda mkuu wa kwanza wa makao makuu ya anga ya juu ya nchi hiyo.

    Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na ikulu ya Marekani, makao makuu hayo yataunganisha nguvu za majeshi, kuhakikisha Marekani inakuwa na uwezo wa kuingia katika anga ya juu na kufanya operesheni katika anga ya juu kwa uhuru bila ya kizuizi chochote.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako