• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Utaratibu wa uteuzi wa Mkaguzi Mkuu mpya kuanzia Septemba 23

    (GMT+08:00) 2019-08-30 19:55:42
    Jopo la kuwapiga msasa watakaotuma maombi ya kujaza nafasi ya Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali litateuliwa mnamo Septemba 23, 2019.

    Rais Uhuru Kenyatta ambaye alianzisha mchakato wa uteuzi wa atakayechukua wadhifa huo kwa kutangaza wazi nafasi hiyo kupitia notisi kwenye gazeti rasmi la serikali Jumanne siku moja baada ya Edward Ouko kukamilisha muhula wake wa kuhudumu Jumatatu.

    Rais atateua mwenyekiti wa jopo hilo la uteuzi pamoja na wanachama ambao watatoka Hazina ya Kitaifa, Ofisi ya Mwanasheria Mkuu, Wizara ya Utumishi wa Umma, Taasisi ya Wahasibu Nchini (ICPA), Muungano wa Mashirika ya Kitaalamu Afrika Mashariki na Chama cha Wanasheria Nchini (LSK).

    Hii ni kulingana na Sehemu ya 11 (5) ya Sheria kuhusu Ukaguzi wa Asasi za Umma ya 2015 (Public Audit Act 2015).

    Kwa mujibu wa notisi hiyo kwenye gazeti rasmi la serikali, wale ambao wanataka kushikilia wadhifa huo wamepewa muda wa hadi Septemba 9, 2019, kuwasilisha maombi yao.

    Bw Ouko aliteuliwa kuwa Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali wa kwanza chini ya Katiba ya sasa, mnamo Agosti 27, 2011, na Rais mstaafu Mwai Kibaki.

    Kulingana na sehemu ya 11 (3) ya Sheria kuhusu Ukaguzi wa Asasi za Umma, wanaotuma maombi kwa uteuzi kuwa Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali wanahitajika kuyawasilisha kwa Tume ya Utumishi wa Umma (PSC) au kupitia mashirika au makundi yanayounga mkono azma zao.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako