• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Tanzania yaanza kukusanya maoni kutoka kwa wadau wa usafirishaji wa nchi kavu

    (GMT+08:00) 2019-08-30 19:56:27

    Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano nchini Tanzania imeanza kukusanya maoni kutoka kwa wadau wa usafirishaji wa nchi kavu, ili kusaidia kuboresha rasimu nane za kanuni zilizoandaliwa na wizara, ili kuleta mabadiliko chanya katika sekta ya uchukuzi.

    Akizungumza na wadau wa usafirishaji pamoja na Mamlaka ya Usafiri wa Ardhini (Latra), Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Dk. Leonard Chamriho, amewataka kutoa maoni yao yatakayosaidia kuondoa baadhi ya vikwazo vya usafiri wa ardhini.

    Chamriho alisema hakuna sababu ya kuhofia kutoa maoni kuhusiana na kile wanachoona kinafaa katika uboreshaji wa kanuni hizo.

    Alizitaja kanuni hizo kuwa ni kuwathibitisha madereva na usajili wa wafanyakazi na vyombo vya biashara, kuwathibitisha madereva na kuwasajili wafanyakazi wa treni, tozo, ukodishaji wa magari madogo na pikipiki, kushughulikia mapitio ya uamuzi ya mamlaka, magari ya abiria na magari ya mizigo.

    Chamriho ameongeza kuwa kupitia kanuni hizo, wadau wanatakiwa kushiriki kikamilifu kutoa maoni yao kwa lengo la kupata kanuni ambazo ni bora na zitakazotekelezeka kwa urahisi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako