• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Watu watano wauawa na wengine 21 kujeruhiwa kwenye shambulizi la kufyatua risasi Texas nchini Marekani

    (GMT+08:00) 2019-09-01 17:13:38

    Watu watano wameuawa na wengine 21 kujeruhiwa kwenye shambulizi la kufyatua risasi lilitokoea katika eneo la Midland-Odessa jimboni Texas nchini Marekani.

    Kwa mujibu wa Idara ya polisi ya Odessa, mfyatuaji risasi mmoja mzungu ambaye yupo kwenye miaka ya 30 ni miongoni mwa waliouawa. Hata hivyo polisi hawakutaja jina la mshambuliaji au sababu ya kushambulia. Akifafanua tukio hilo kwa wanahabari, Mkuu wa Polisi wa Odessa Michael Gerke amesema ufyatuaji risasi ulianza Jumamosi mchana wakati askari wa Idara ya Usalama wa Umma alipojaribu kuzuia gari aina ya Honda. Baada ya kulisimamisha gari hilo, askari huyo alipigwa risasi na mwenye gari, baadaye gari hilo lilielekea magharibi kwenye mji wa Odessa, na dereva kuanza kuwafyatulia risasi watu ovyo. Amesema watatu kati ya waliojeruhiwa ni maafisa wa polisi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako