• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • UM wasema hatua imara zahitajika ili kusitisha upotevu wa viumbe anuwai

    (GMT+08:00) 2019-09-02 08:14:08

    Katibu mtendaji wa Sekretarieti ya Mkataba wa Umoja wa Mataifa Khusu Uanuwai wa Viumbe CBD, Cristian Pasca Palmer amesema nchi zinapaswa kuchukua hatua imara ili kusitisha upotevu wa viumbe anuwai ambao umekuwa ukiongezeka kwa kasi kutokana na mabadiliko ya tabia nchi na shughuli zisizo endelevu zinazohusiana na upanuzi wa kasi wa miji.

    Akiongea mwishoni mwa mkutano wa Mkataba wa Umoja wa Mataifa Khusu Uanuwai wa Viumbe huko Nairobi, Bi. Palmer amesema ili kuongeza uhifadhi wa viumbe anuwai nchi zinapaswa kujumuisha juhudi za dunia za kutokomeza umasikini, njaa na magonjwa. Na kubainisha kuwa kuna dharura ya kuwa na makubaliano mapya ya pande nyingi ili kuhimiza uhifadhi wa viumbe anuwai kama njia ya kufikia maendeleo endelevu.

    Mkutano huo uliowaleta pamoja watunga sera, wanasayansi na wapiga kampeni, unaanza kujadili muongozo mpya wa kuimarisha uhifadhi wa viumbe anuwai, ambao unatarajiwa kupitishwa na pande 196 za CBD katika mkutano uliopangwa kufanyika Oktoba 2020 mjini Kunming, kusini magharibi mwa China.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako