• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Wabunge Wahafidhina wanaopinga Brexit isiyo na makubaliano kufanya mkutano na Waziri mkuu wa Uingereza

    (GMT+08:00) 2019-09-02 08:21:39

    Mawaziri kadhaa wa zamani wa Uingereza ambao pia ni wabunge wahafidhina wanaopinga Brexit isiyo na makubaliano, wanatarajiwa kufanya mkutano na waziri mkuu wa Uingereza Bw. Boris Johnson leo Jumatatu, ambayo ni mwanzo wa wiki muhimu kwa siasa za nchi hiyo.

    Mkutano huo uliopangwa, ulitangazwa wakati aliyekuwa waziri wa sheria David Gauke aliposema Jumapili kuwa anaamini maslahi ya taifa yanapaswa kupewa kipaumbele hata kama hatachaguliwa kwenye uchaguzi ujao.

    Bw. Gauke ni miongoni mwa mawaziri kadhaa waliojiuzulu baada ya Bw. Johnson kuwa waziri mkuu, na pia ni mmoja kati ya mawaziri wa zamani watakaounga mkono hatua ya bunge wiki hii kupinga Brexit isiyo na makubaliano.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako