• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Michuano ya Bara Afrika- Malkia Strikers iko tayari kufanya kweli

  (GMT+08:00) 2019-09-02 08:46:17

  Baada ya kuwapiga mara mbili mahasimu wao wakubwa Cameroon na kutwaa ubingwa wa Voliboli kwa wanawake kwenye mchezo wa bara la Afrika (All African Games) nchini Morocco, timu ya voliboli ya wanawake ya Kenya Malkia Strikers sasa inaelekeza macho yake kwenye michuano ya kombe la dunia itakayofanyika Septemba 14-29 nchini Japan.

  Kenya ambayo sasa inajivunia mataji matano ya wanawake ya African Games, pamoja na Cameroon zitawakilisha Bara la Afrika katika michuano hiyo ya dunia. Malkia Strikers itamenyana na Marekani (Septemba 14), Uholanzi (Septemba 15), Serbia (Septemba 16), Brazil (Septemba 18) na Argentina (Septemba 19) mjini Hamamatsu, na kisha Itaelekea mjini Sapporo kupepetana na Jamhuri ya Dominican (Septemba 22), Japan (Septemba 23) na Uchina (Septemba 24).

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako