• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Waziri Mkuu wa Sudan apinga kuingilia uteuzi wa mawaziri wa serikali ya mpito

  (GMT+08:00) 2019-09-02 09:12:45

  Waziri Mkuu wa Sudan Bw. Abdalla Hamdok ametoa taarifa akisistiza kuwa anapinga kabisa jaribio lolote lile la kuingilia kati au kushawishi uteuzi wake wa mawaziri wa serikali ya mpito.

  Bw. Hamdok amekosoa kile alichokitaja kama orodha iliyo chini ya msingi wa upendeleo, iliyowasilishwa na Muungano wa Uhuru na Mabadiliko, na kusisitiza vigezo vilivyowekwa vya kuchagua mawaziri wa serikali wanaoweza kuiongoza nchi kuelekea kwenye usalama. Ameongeza kuwa mawaziri saba tu hadi sasa wamechaguliwa kutoka kwenye orodha ya wateule, na kuutaka Muungano wa Uhuru na Mabadiliko kuwasilisha orodha nyingine mbadala ya wagombea ndani ya saa 24.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako