• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Rais wa Zimbabwe atarajia kuhotubia maandamano ya kupinga vikwazo

  (GMT+08:00) 2019-09-02 19:30:27

  Rais Emmerson Mnangagwa wa Zimbabwe anatarajiwa kuwahotubia wafuasi wa chama tawala cha ZANU-PF wanaopanga kukusanyika mjni Harare kwa ajili ya matembezi ya mshikamano ya kupinga vikwazo Alhamisi wiki hii.

  Gazeti la Herald limeripoti kuwa, matembezi hayo yanalenga kuziunga mkono nchi wanachama wa Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika SADC kwa kutoa wito kuondoa vikawzo vilivyowekwa na Marekani na Umoja wa Ulaya tangu miaka ya mapema ya karne hii.

  Serikali ya Zimbabwe inalalamika kuwa, vikwazo hivyo vimeleta athari mbaya kwenye uchumi wa nchi na kuleta mateso kwa watu.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako