• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Waziri mkuu wa Uingereza asema hatautaka Umoja wa Ulaya kuahirisha Brexit

    (GMT+08:00) 2019-09-03 08:54:47

    Waziri mkuu wa Uingereza Bw. Boris Johnson amesema, hakuna njia yoyote ile itakayomfanya autake Umoja wa Ulaya kuahirisha nchi yake kujitoa kwenye umoja huo. Pia amesema, anataka kila mmoja afahamu kuwa wanajitoa Oktoba 31, hakuna mjadala.

    Ingawa vyombo vya habari vilikisia kuwa Bw. Johnson atatangaza kutoa wito au kutishia kufanya tena uchaguzi mkuu, lakini Bw. Johnson amesema hataki kufanya uchaguzi. Badala yake, amewataka wabunge wahafidhina wanaopinga Brexit isiyo na makubaliano kutozuia fursa za Uingereza kujitoa kwenye Umoja wa Ulaya bila makubaliano.

    Kabla ya taarifa ya Bw. Johnson, mwenyekiti wa kamati ya Brexit ya baraza la makabwela la Uingereza Bw. Hilary Benn ametoa maelezo kuhusu mswada utakaowasilishwa na wabunge wakati bunge litakapofunguliwa tena leo baada ya mapumziko ya majira ya joto. Mswada huo unalenga kupitisha haraka sheria bungeni ya kumzuia Bw. Johnson kuitoa Uingereza kwenye Umoja wa Ulaya bila ya makubaliano na kutandika njia ya kuongeza muda wa Brexit hadi Januari 31, mwaka 2020.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako