• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Kenya yasimamisha utafutaji baada ya kupata miili yote 7

  (GMT+08:00) 2019-09-03 09:23:06

  Mamlaka ya Wanyamapori Kenya KWS limesema, kazi ya utafutaji na uokoaji imesimamishwa baada ya miili yote 7 ya watalii na mwongozaji wao kupatikana.

  KWS imesema kwenye taarifa kuwa, watalii sita wa Kenya na mmoja wa India walisombwa na mafuriko ya ghafla wakati walipotalii kwenye korongo la Hifadhi ya Taifa ya Hell's Gate huko Naivasha, kilomita 90 kutoka Nairobi. Pia imesema korongo hilo limefungwa kwa muda usiojulikana kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako