• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Afisa mkuu mtendaji wa Hong Kong akanusha kutoa ombi la kujiuzulu

  (GMT+08:00) 2019-09-03 19:15:47

  Mkuu wa serikali ya mkoa wa utawala maalum wa Hong Kong Bibi Carrie Lam amesema, hakuwahi kutoa ombi la kujiuzulu kwa serikali kuu ya China.

  Bibi Lam amesema, kuendelea na nafasi yake ni chaguo lake mwenyewe, na kusisitiza kuwa, yeye na timu yake wanapaswa kuendelea kuwepo na kuwatumikia na kuwasaidia watu wa Hong Kong kukabialiana na kipindi hiki kigumu.

  Bibi Lam pia amesema, watu wengi wa Hong Kong na serikali yake wanakubaliana kuwa, kazi muhimu kwa sasa ni kusimamisha mapambano na kurudisha utulivu mkoani humo. Amesema, lengo hilo litatimizwa kwa kupitia utekelezaji wa sheria. Ameongeza kuwa, kufanya mazungumzo hasa na vijana ni njia mwafaka zaidi ya kubadilisha tofauti zilizopo katika jamii ya Hong Kong.

  Aidha, msemaji wa ofisi ya mambo ya Hong Kong na Macao ya Baraza kuu la China Bw. Yang Guang amesema, lengo la waandamanaji kadhaa mkoani Hong Kong ni kuanzisha vurugu mkoani humo. Serikali kuu ya China inamuunga mkono Bibi Carrie Lam kushirikiana na watu wa Hong Kong kutatua masuala ya uchumi na jamii mkoani humo.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako