• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kenya: Wakulima kuanzisha viwanda vya kusaga unga

    (GMT+08:00) 2019-09-03 19:24:08
    Wakulima wa mahindi katika eneo la kaskaini mwa bonde la ufa nchini Kenya wameanza mchakato wa kuanzisha viwanda vya kusaga unga ili kukomesha mzozo wa bei wa bidhaa hiyo uliodumu kwa miaka mingi.

    Wakulima hao wamesema wamekuwa wakipata hasara kubwa, kucheleweshwa malipo, na pia kulaghaiwa na madalali.

    Chama cha wakuza nafaka cha eneo hilo kimesema kuwa vyama vya wakulima 100 tayari vimeonesha nia ya kununua hisa kwenye viwanda vitakavyoanzishwa kwaka ujao.

    Mweka hazina wa vyama hivyo David Kiberenge amesema viwanda vitatu vitahudumia wakulima kwenye kaunti za Uasin Gishu, Trans Nzoia, Nandi na Elgeyo Marakwet.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako