• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rwanda: Benki ya dunia yaipa Rwanda dola milioni 125 za kuendeleza sekt aya umeme

    (GMT+08:00) 2019-09-03 19:25:41

    Serikali ya Rwanda na Benki ya Dunia zimetia saini makubaliano ya mkopo ya dola milioni 125 ambayo za kusaidia upanuzi wa huduma za umeme nchini.

    Pesa hizo zinazoelekezwa kwa sera mpya ya Operesheni ya Maendeleo ya Nishati ya Rwanda (DPO) ni za tatu na mwisho chini ya mpango wa dola milioni 375 wenye lengo la kusaidia malengo ya sekta ya nishati yaliyomo kwenye Mkakati wa kitaifa wa mabadiliko (NST1).

    Ya kwanza ilipitishwa mnamo Desemba 2017.

    Waziri wa Fedha na Mipango ya Uchumi Dk.Uziel Ndagijimana alisema kuwa makubaliano hayo yamechangia sana kuboresha sekta ya nishati haswa katika upatikanaji.

    Meneja Benki ya Dunia, nchini humo Said Yasser El-Gammal, aliwaambia waandishi wa habari katika hafla ya utiaji saini huko Kigali kwamba pesa hizo tayari zilitumika vizuri kwenye utekelezaji wa kazi za sera ya maendeleo.

    Rwanda inakusudia upatikanaji wa umeme wa asilimia 61 ifikapo 2020.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako