• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Baraza la Usalama kujadili ushirikiano na mashirika ya kikanda na masuala ya Afrika mwezi huu

  (GMT+08:00) 2019-09-04 08:26:23

  Mwenyekiti wa mwezi wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa Vassily Nebenzia amesema Baraza hilo litajadili Ushirikiano wa Umoja wa Mataifa na mashirika ya kikanda na kusuluhisha matatizo ya Afrika kwenye mikutano miwili itakaofanyika mwezi huu.

  Akiongea na wanahabari Bw Nebenzia ambaye pia ni balozi wa Russia katika Umoja wa Mataifa amesema mikutano hiyo ni ya ngazi ya mawaziri pamoja na ushirikiano kati Umoja wa Mataifa na mashirika ya kikanda, pamoja na kuhusu amani na usalama katika Afrika.

  Waziri wa mambo ya nje wa Russia Sergey Lavrov anatarajiwa kuwa mwenyekiti wa mikutano hiyo na katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres anaweza kuhutubia katika mikutano yote miwili.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako