• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • SOKA: Uganda Cranes yatangaza kikosi chake kitakachoivaa Harambee Stars

  (GMT+08:00) 2019-09-04 08:30:40

  Kocha wa timu ya taifa ya Uganda (Uganda Cranes) Abdallah Mubiru ametaka kikosi cha wachezaji 25 cha timu hiyo kitakachokutana na timu ya taifa ya Kenya (Harambee Stars) kwenye mechi ya kirafiki ya kimataifa itakayopigwa jijini Nairobi Septemba 8.

  Mubiru amewajumuisha wachezaji walioshiriki michuano ya mataifa ya Afrika (AFCON) yaliyomalizika nchini Misri.

  Shirikisho la soka la Uganda (FUFA) limesema linatumia michezo ya kirafiki ya kimataifa kukiandaa kikosi chao kwa mchezo wa kufuzu michuano ya CHAN 2020 kwa wachezaji wa ndani dhidi ya Burundi na ya kufuzu mataifa ya Afrika (AFCON 2021) ambayo inatarajiwa kuanza mwezi Novemba mwaka huu huku Uganda wakipangwa kucheza na Burkina Faso na Malawi.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako