• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Watoto warudi shuleni kwenye maeneo yanayokumbwa na Ebola DRC

    (GMT+08:00) 2019-09-04 08:56:54

    Mwakilishi wa Mfuko wa Kuwahudumia Watoto wa Umoja wa Mataifa (UNICEF) nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo Edouard Beigbeder jana alisema, shule zimefunguliwa upya kwa watoto takriban milioni 2 wanaoishi kwenye maeneo yanayoathiriwa na mlipuko wa ugonjwa wa Ebola mashariki mwa nchi hiyo.

    Beigbeder amesema, ugonjwa wa Ebola umeleta madhara makubwa kwa familia na jamii za huko. Amesema kuhakikisha watoto hao wanakwenda shule zilizo salama, zinazolindwa na za kukaribisha ni muhimu ili kuwasaidia warudi kwenye hali ya kawaida na kuendelea na masomo yao.

    Kwa mujibu wa UNICEF kuna shule 6,509 za msingi na sekondari kwenye maeneo yaliyoathiriwa na ugonjwa wa Ebola katika majimbo ya Ituri, Kivu Kaskazini na Kivu Kusini, kati yao kuna shule 3,800 zilizoko kwenye maeneo yenye hatari kubwa, lakini shule nyingi zimefunguliwa kwa muhula mpya.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako