• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Waziri mkuu wa Sudan asisitiza umuhimu wa kuiondoa Sudan kwenye orodha ya ugaidi ya Marekani

    (GMT+08:00) 2019-09-04 08:57:35

    Waziri mkuu wa Sudan Abdalla Hamdok jana alisisitiza umuhimu wa kuiondoa Sudan kwenye orodha ya Marekani ya nchi zinazofadhili ugaidi.

    Hamdok ameyasema hayo alipokutana na waziri wa mambo ya nje wa Ujerumani Heiko Maas ambaye yuko ziarani nchini Sudan. Amesisitiza kuwa ni lazima kuiondoa Sudan kwenye orodha hiyo, na Sudan inatarajia kupata maendeleo mapema kwenye suala hilo.

    Vielvile amesema Sudan inakabiliwa na changamoto kubwa za kiuchumi, lakini zinaweza kuondolewa. Amesema kwa sasa wanapaswa kukabiliana na kuzorota kwa kiwango cha ubadilishaji wa fedha, kuzuia mfumuko wa bei na kurudisha imani kwenye sekta ya benki.

    Kwa upande wake Bw. Maas ameahidi kuwa Ujerumani itaendelea kuiunga mkono Sudan, pia kuitaka jumuiya ya kimataifa iunge mkono juhudi za Sudan za kuboresha uchumi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako