• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Eneo la biashara huria la Afrika kutekelezwa mwanzoni mwa 2020

  (GMT+08:00) 2019-09-04 09:23:03

  Eneo la biashara huria la pande tatu la Afrika TFTA litatekelezwa mapema mwaka 2020.

  Mkurugenzi wa biashara na forodha wa Soko la Pamoja la Mashariki na Kusini mwa Afrika COMESA Francis Mangeni jana alisema mpaka sasa nchi tano zimethibitishwa na TFTA, ambayo inaunganisha jumuiya za kibiashara za COMESA, Jumuiya ya Afrika Mashariki EAC na SADC. Amesema nchi nyingine 11 zinatarajiwa kuingia kwenye makubaliano na TFTA kabla ya mwishoni mwa mwaka huu ili eneo hilo lianze kutekelezwa.

  Habari nyingine zinasema, katibu mkuu wa COMESA Bw. George Lipimile amesema sera za kujilinda kibiashara zinaharibu uchumi wa kanda hiyo. Amesema, makampuni yakikosa ushindani kutoka kwa makampuni ya nchi za nje, yatashindwa kushiriki kwenye biashara ya kikanda na ya kimataifa. Nchi mbalimbali hazipaswi kulinda sekta zao za viwanda za ndani kwa kupitia vikwazo vya biashara au kiwango cha juu cha ushuru, kwa sababu italeta hasara kwa wateja wao kwa muda mrefu.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako