• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Kundi la upinzani Sudan Kusini lakana kusajili wapiganaji kutoka Uganda

  (GMT+08:00) 2019-09-04 09:39:11

  Kundi kuu la upinzani nchini Sudan Kusini SPLA-IO jana lilikanusha kusajili wapiganaji kutoka nchi jirani ya Uganda.

  Naibu msemaji wa kundi hilo Lam Paul Gabriel amekanusha ripoti zilizotolewa hivi karibuni na vyombo vya habari vya Uganda kuwa SPLA-IO linawashawishi kwa pesa vijana kwenye sehemu ya kaskazini mwa Uganda kujiunga na kundi hilo.

  SPLA-IO limekuwa likituhumiwa kuwaingiza maofisa wa Uganda kwenye vyeo vyake ambao hadi sasa wameshasajili vijana 30 kutoka eneo la kaskazini la Gulu mkoani Ikweta Mashariki karibu na mpaka wa Sudan Kusini.

  Msemaji huyo amsema SPLA-IO linashiriki katika utekelezaji wa mipango ya mpito ya usalama pamoja na serikali ya Sudan Kusini na vikosi vyake vyote viko kambini kusubiri kuchunguzwa na kuandikishwa.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako