• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Iran kuchukua hatua ya tatu ya kupunguza ahadi zake za nyuklia

    (GMT+08:00) 2019-09-04 19:03:09

    Rais Hassan Rouhani wa Iran amesema nchi yake itachukua hatua ya tatu ya kupunguza ahadi zake za makubaliano ya nyuklia ya mwaka 2015.

    Akinukuliwa na Televisheni ya taifa IRIB, Rouhani amesema licha ya maendeleo yaliyopatikana kwenye mazungumzo kati ya Iran na pande za Ulaya kuhusu makubaliano ya nyuklia, hadi sasa makubaliano ya mwisho bado hayajafikiwa. Hivyo amesema Iran itachukua hatua ya kupunguza ahadi zake kwenye makubaliano hayo, na itatangaza hivi karibuni.

    Amesema hatua ya tatu ni muhimu sana na itaharakisha shughuli za Shirika la Nguvu za Atomi la Iran.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako