• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Sportpesa yaruhusiwa kerejelea biashara

    (GMT+08:00) 2019-09-04 19:54:56
    Kampuni ya Sportpesa imejiunga na baadhi ya kampuni zingine za kamari nchini Kenya zilizoruhusiwa kurejelea kutekeleza shughuli zao za bahati nasibu baada ya kuzuiliwa kufanya hivyo kwa muda.

    Mamlaka ya Ukusanyaji Ushuru nchini Kenya KRA iliidhinisha kurudishwa kwa leseni ya kampuni hiyo baada ya kuzimwa kwa muda wa miezi miwili.

    Kampuni hiyo ilisema kuwa imekuwa ikijadiliana na washikadau, na pia wadhibiti wa ushuru kutoka kwa serikali kuhusu leseni yake, majadiliano ambayo yalinuia kueleza vyema madhumuni na sheria ambazo zinahitajiwa kufuatwa, ikiwemo ile ya kulipa ushuru.

    Taarifa hiyo ilizidi kueleza kuwa kampuni hiyo inawashukuru wafanyikazi na mashabiki wake wote, na hivi karibuni, itatoa ujumbe kueleza itakapokua ikirejelea shughli zake.

    Kampuni hiyo ya kamari ilikua miongoni mwa zingine zikiwemo Betin, Betway, Betpawa, Premierbet ambazo leseni zao zilifutiliwa mbali na serikali mwezi Julai, kwa shutuma za kutolipa ushuru.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako