• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Carrie Lam atoa hatua nne za kumaliza hali ya msukosuko ya Hong Kong

  (GMT+08:00) 2019-09-04 20:06:45

  Mkuu wa mkoa wa utawala maalumu wa Hong Kong bibi Carrie Lam ametoa hotuba kupitia televisheni akitoa hatua nne za kumaliza hali ya msukosuko mkoni humo.

  Hatua hizo ni pamoja na kufuta mswada wa marekebisho ya sheria, kuunga mkono kwa nguvu zote kazi za polisi, maofisa wa ngazi ya juu kufanya mazungumzo ya ana kwa ana na raia kuanzia mwezi huu, na kuwaalika viongozi wa jamii, wataalamu na wasomi kufanya utafiti kuhusu taabu za kijamii na kutoa mapendekezo kwa serikali.

  Bibi Lam amesisitiza kuwa vurugu na vitendo vya kimabavu zinatikisa msingi wa utawala wa kisheria wa Hong Kong, na sasa kazi muhimu zaidi ni kurejesha utaratibu wa kijamii.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako