• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Uganda-Kampuni ya UCL yatarajia kupata hasara

    (GMT+08:00) 2019-09-05 20:19:56
    Kampuni ya kutengeneza vifaa vya ujenzi na paa za nyumba nchini Uganda ,Uganda Clays Limited,imetoa onyo kwa wamiliki wa hisa kuwa huenda ikapata hasara katika matokeo yake ya nusu mwaka.

    Katika notisi iliyochapishwa jana,Mkurugenzi Mkuu wa UCL,Bw George Inholo, alisema kampuni hiyo inatarajia kupata hasara kwenye utendaji wake katika kipindi cha kuanzia mwezi januari hadi Juni 2019 kutokana na changamoto za uendeshaji.

    Katika kipindi sawa na hicho mwaka jana kampuni hiyo ilipata faida.

    Hasara hiyo,Inholo alisema,imetokana na kupungua kwa mapato,na hatimaye kuathiri uendeshaji.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako