• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Tanzania-Mtaalamu wa masuala ya usafiri wa meli ampongeza Rais Magufuli kwa kazi anazofanya katika sekta ya bandari na meli

  (GMT+08:00) 2019-09-05 20:25:21

  Mtaalamu wa Kimataifa katika masuala ya usafirishaji bidhaa kwa njia ya meli (FICS) Julius Nguhulla amesema ataendelea kumshauri Rais John Pombe Magufuli kuhusu sekta ya meli nchini Tanzania kwa maslahi ya wananchi wote.

  Nguhulla amesema Juni 3 mwaka huu ,alimuandikia barua ya kumpongeza Rais Magufuli kwa kazi nzuri anazofanya kuhusu sekta ya bandari na meli ikiwa ni pamoja na kuanzishwa kwa Shirika la Meli Tanzania (TASAC).

  Nguhulla ameyasema hayo jijini Dar es Salaam wakati akizungumza na waandishi wa habari na kusema kuwa lengo ni kuisaidia sekta ya usafiri wa meli katika kukuza uchumi wa taifa.

  Amesema katika barua hiyo,alimuomba Rais Magufuli kuishauri Mamlaka husika kuhusu umuhimu wa tozo,utoaji mizigo na jinsi zilivyokuwa zikichangia pato kwa taifa.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako