• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Museveni asema Uganda ni salama kwa wawekezaji

  (GMT+08:00) 2019-09-06 19:25:27

  Rais Yoweri Museveni wa Uganda amesema ni mahala salama zaidi kwa yeyote anayetaka kuwekeza nchini humo. Museveni amewataka wawekezaji watumie fursa hiyo na kuwekeza nchini humo. Amesema Uganda hivi sasa ina zaidi ya wakimbizi milioni 1.4 kutoka nchi jirani ambao wamekuwa wakiishi nchini humo na kufanya biashara zao bila wasiwasi. Aidha Museveni ameongeza kuwa tayari Uganda imeweka miundo mbinu mizuri ili kurahisisha shughuli za kibiashara nchini humo. Amesema sasa wawekezaji wanaweza kufanya shughuli zao bila vikwazo vyovyote. Alikuwa akisema hayo kwenye mkutano na wawekezaji katika mji wa Cape Town nchini Afrika Kusini ambako mkutano wa kimataifa wa kiuchumi unaendelea hivi sasa.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako