• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Pande mbalimbali zatakiwa kutetea mazungumzo na ushirikiano kuhusu haki za binadamu badala ya kufanya mapambano

    (GMT+08:00) 2019-09-07 17:57:15

    Balozi wa China katika ofisi za Umoja wa Mataifa huko Geneva Bw. Chen Xu jana alifahamisha msimamo na maoni ya China kuhusu kazi ya ulinzi wa haki za binadamu duniani.

    Akiongea na wanahabari, kabla ya kufunguliwa kwa mkutano wa 42 wa Baraza la wakurugenzi la Haki za binadamu la Umoja wa Mataifa, balozi Chen alisema, China inapenda kujiunga na pande nyingine mbalimbali katika kulinda kithabiti mfumo shirikishi ambao kiini chake ni Umoja wa Mataifa, kutetea ushirikishi na kulinda usawa na haki. China pia inatumai pande mbalimbali zitatetea kufanya mazungumzo na ushirikiano, kutofanya mapambano; kuhimiza kwa uwiano hali ya haki za binadamu za aina mbalimbali, kuheshimu wananchi wa nchi mbalimbali wachague njia yao ya kuendeleza haki za binadamu, kutowalazimisha wengine wafuate vigezo vyao, na kuhimiza kazi ya kutatua matatizo ya haki za binadamu duniani iendelee kwa usawa na haki zaidi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako