• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mawaziri wa mambo ya nje wa China, Afghanistan na Pakistan wafanya mazungumzo

    (GMT+08:00) 2019-09-08 17:14:41

    Mazungumzo ya 3 ya mawaziri wa mambo ya nje wa China, Afghanistan na Pakistan yamefanyika huko Islamabad nchini Pakistan.

    Mawaziri hao wamefikia makubaliano ya kuhimiza Afghanistan kutimiza amani na utulivu wa kudumu kupitia mchakato wa maafikiano unaoongozwa na kusimamiwa na watu wa Afghanistan, kuanzisha miradi ya miundombinu ya mawasiliano kati ya nchi hizo tatu kwa kufanya ushirikiano na mashirika ya fedha ya kimataifa ikiwemo Benki ya Dunia, na kupitia orodha ya kwanza ya shughuli zitakazotekelezwa ya makubaliano ya kupambana na ugaidi kwa nchi hizo tatu. Mawaziri hao pia wamekubaliana kufanya mazungumzo ya 4 kati yao nchini China mwaka kesho.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako