• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Mawaziri wa serikali ya mpito ya Sudan waapishwa

  (GMT+08:00) 2019-09-09 08:37:07

  Mawaziri wa serikali ya mpito ya Sudan wameapishwa jana Jumapili mjini Khartoum mbele ye mwenyekiti wa Baraza la Utawala Abdel-Fattah Al-Burhan.

  Mawaziri wote 18 walikula kiapo cha kikatiba mbele ya Bw. Al-Burhan akiwa pamoja na waziri mkuu Abdalla Hamdok, na mawaziri wawili wanatarajiwa kuteuliwa baadaye kuongoza Wizara ya Miundombinu na Uchukuzi, na Wizara ya Mifugo na Uvuvi.

  Kutokana na amri ya kikatiba iliyotolewa na mwenyekiti wa Baraza la Utawala, Alhamisi iliyopita, Waziri mkuu wa Sudan Bw. Hamdok alitangaza kuundwa kwa baraza la mawaziri la mpito, ambalo ni la kwanza kuundwa baada ya rais wa zamani Omar al-Bashir kuondolewa madarakani.

  Habari nyingine zinasema, waziri wa fedha Bw. Ibrahim Elbadawi jana alitangaza mpango wa kiuchumi utakaotekelezwa kwa siku 200 kwa lengo la kutatua masuala ya dharura yanayoukabili uchumi wa Sudan.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako