• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Aliyekuwa Rais wa Zimbabwe Bw. Robert Mugabe kuzikwa Jumapili

  (GMT+08:00) 2019-09-09 19:42:07

  Taarifa iliyotolewa na serikali ya Zimbabwe imesema aliyekuwa rais wa Zimbabwe Bw. Robert Mugabe aliyefariki nchini Singapore akiwa na umri wa miaka 96 atazikwa Jumapili nchini Zimbabwe.

  Wizara ya mambo ya nje ya Zimbabwe imesema kutakuwa na shughuli ya kuaga mwili katika uwanja wa taifa, kabla ya kuzikwa siku inayofuata. Taarifa imesema wakuu wa nchi na serikali wanaopenda kuhudhuria shughuli za mazishi wanatakiwa kufika mjini Harare Ijumaa.

  Serikali pia imesema itatuma ujumbe wa ngazi ya juu nchini Singapore unaoongozwa na makamu wa Rais Bw. Kembo Mohadi, ili kuuchukua mwili wa Bw. Mugabe na unatarajiwa kufika nchini Zimbabwe Jumatano wiki hii.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako