• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rais Xi Jinping atuma salama za pongezi kwa kiongozi wa Korea Kaskazini kufuatia maadhimisho ya miaka 71 ya kuanzishwa kwa nchi hiyo

    (GMT+08:00) 2019-09-09 19:52:17

    Rais Xi Jinping wa China leo ametuma salama za pongezi kwa kiongozi wa Korea Kaskazini Kim Jong-un kufuatia kuadhimisha miaka 71 ya kuanzishwa kwa Korea Kaskazini.

    Kwenye salamu zake za pongezi rais Xi kwa niaba ya Chama cha Kikomunisti cha China, serikali ya China na watu wake, amemtakia kila la heri Bw. Kim Jong-un pamoja na Chama cha Leba cha Korea Kaskazini, serikali na watu wa Korea Kaskazini.

    Rais Xi amesema katika miaka 71 tangu Korea Kaskazini ianzishwe, chini ya uongozi wa Chama cha Leba, watu wa nchi hiyo wanahimiza mapinduzi ya Ujamaa na mambo ya ujenzi kusonga mbele. Amesema China inapenda kudumisha urafiki kati ya nchi mbili na kuhimiza uhusiano wa ushirikiano upate maendeleo zaidi, ili kuwaendeleza zaidi wananchi wa nchi hizi mbili.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako